Alhamisi, 7 Aprili 2016

PUMU NA MAELEZO YA KUITIBU KIASILI





Katika somo hili tutajadili dawa mbadala 13 zinazoweza kuzuia au kutibu kabisa tatizo la pumu mwilini. Chagua unayoona ni rahisi kuipata na uitumie. Unaweza kutumia dawa 2 au 3 kwa pamoja. Endelea kusoma.
Vitu vinachosababisha au kuamsha Pumu
  • Aleji/mzio
  • Tumbaku/sigara
  • Sabubu za kimazingira kama uharibifu wa hewa sababu ya viwanda
  • Uzito uliozidi
  • Mfadhaiko/Stress, sononeko, na huzuni
  • Kurithi
  • Maambukizi mapafuni wakati wa utotoni
  • Kuzaliwa mapema/njiti
  • Baadhi ya vyakula kama samaki, soya, mayai, korosho nk
  • Mazoezi
  • Kiungulia
Dalili za Pumu
  • Kupata shida wakati wa kupumua
  • Sauti ya kukoroma wakati unapumua
  • Kikohozi
  • Msongamano kifuani
  • Kujisikia umechoka wakati ukifanya kazi yoyote ya nguvu
  • Homa na vikohozi vya mara kwa mara
  • Kukosa utulivu katika usingizi

Dawa mbadala 13 zinazotibu Pumu

1. Kitunguu swaumu
Kitunguu swaumu
Kitunguu swaumu
Chukua punje 5 hadi 6, menya na ukate vipande vidogo vidogo lakini siyo vidogo sana na uchemshe kwenye moto na maji kikombe kimoja (robo lita), ongeza kijiko kikubwa kimoja cha asali mbichi ndani yake na uache kwenye moto kama dakika 5. Ipua na unywe kwa pamoja kutwa mara 2 hadi utakapopona.

2. Tangawizi
dawa mbadala zinazotibu pumu
Tangawizi
Tangawizi pia ina faida nyingi katika mwili wako na afya yako. Tengeneza juisi robo lita yenye mchanganyiko wa tangawizi, komamanga na asali. Kunywa mchanganyiko huo kutwa mara 2 au 3 kwa matokeo ya haraka.
Namna nyingine ni kuchukua kijiko kikubwa kimoja cha juisi ya tangawizi (majimaji ya tangawizi) changanya na kijiko kikubwa kimoja cha asali na vijiko vikubwa 2 vya mbegu kavu za uwatu na uuache mchanganyiko huu kwa usiku mmoja. Kunywa mchanganyiko huu kesho yake ili kuondoa sumu kwenye mapafu yako.

3. Mafuta ya mharadali
Mustard OilDawa mbadala 13 zinazotibu pumu

Chukua mafuta kidogo ya mharadali na uchanganye na kafuri (camphor) ndani yake. Jipakae mchanganyiko huu taratibu sehemu yote ya kifua mpaka uone nafuu inajitokeza. Hakikisha unayapasha mafuta kidogo katika moto kabla ya kuanza kujipaka taratibu (masaji) ili kifua kiweze kuhisi au kulipata hilo joto na hatimaye upate uponyaji kwa aharaka zaidi. Fanya zoezi hili wiki 2 hadi 3

4. Mtini (Figs)
Mtini ni dawa nyingine ya asili (home remedy) nzuri dhidi ya pumu. Loweka baadhi ya mitini mikavu ndani ya maji kwa usiku mmoja. Kula huo mtini uliolowekwa kesho yake asubuhi kabla ya kula kitu kingine chochote. Pia kunywa maji hayo yaliyoloweka mtini kwa ajili ya kujitibu pumu au asthma. Fanya hivi kwa wiki 2 hadi 3

5. Mafuta ya mkalitusi
Mafuta ya mkalitusi (Eucalyptus essential oil) yanaweza kupelekea uponyaji wa haraka kwa mtu anayesumbuliwa na pumu. Weka matone machache ya mafuta haya ndani ya kikombe cha maji ya moto na usogeze pua yako karibu na mvuke unaojitokeza na uuvute ndani taratibu. Hii itasaidia kuzifungua pua zilizokuwa zimeziba sababu ya pumu na hivyo hewa inaweza kuanza kuingia na kutoka kirahisi zaidi.

6. Asali
Asalidawa mbadala zinazotibu pumu

Kama unatafuta dawa ya asili ya kutibu pumu basi asali ndiyo dawa bora ya asili inayotibu pumu kuliko dawa nyingine yoyote. Unaweza kutumia kijiko kidogo kimoja cha chai kilichochanganywa na robo lita ya maji ya moto walau mara 2 mpaka 3 kwa siku au unaweza kuwa unanusa ile harufu fresh ya asali mara kadhaa kila siku.
Namna nyingine ni kuchukua kijiko kikubwa kimoja cha asali mbichi changanya na nusu kijiko kimoja cha chai cha mdalasini ya unga na ulambe mchanganyiko huo kila unapoenda kulala kila siku hadi upone.

7. Kitunguu maji
Vitunguu vinajulikana kuwa na sifa ya kutibu uvimbe (inflammatory) na vimethibitika kuwa na msaada mkubwa katika kusafisha njia ya hewa. Kwahiyo kama wewe ni mhanga wa pumu au asthma basi unapaswa kuwa unatumia vitunguu maji kwa wingi kila siku vikiwa vibichi kabisa, vikiwa katika kachumbali au hata vikiwa vimepikwa pamoja na mboga mboga zingine.

8. Matunda na Limau
Matunda kama stroberi, bluberi, papai, na machungwa yameonyesha kuwa na msaada kwa watu wanaosumbuliwa na pumu. Pia limau zina vitamin C na zinatakiwa kutumia sambamba na maji, sukari/asali na chumvi kidogo ya mawe walau mara moja kwa siku kwa majuma kadhaa ili kujitibu ugonjwa huu wa pumu.

9. Samaki
Kula mara kwa mara samaki kama ‘salmon’ (au samoni kwa Kiswahili ni samaki mkubwa mwenye mnofu mwekundu), tuna au jodari, dagaa chumvi wa baharini (sardines) kunaweza kuwa msaada mkubwa sana katika kujitibu tatizo la pumu. Samaki hawa wote huyafanya mapafu yako kuwa safi, salama na yenye nguvu katika kupambana na tatizo la pumu na kuitibu haraka na kwa ufanisi. Ingawa ikiwa hauwezi kula hawa samaki katika hali ya kupikwa basi unaweza kubadili kwa kutumia mafuta yatokanayo na samaki hawa.

10. Zabibubata (Gooseberries/Amla)
dawa mbadala zinazotibu pumu
Zabibubata/Zabibu nyekundu
Zabibubata ni nzuri sana katika kutibu pumu. Ponda ponda zabibubata kadhaa na ongeza asali kidogo ndani yake, tumia mchanganyiko huu kila siku na ukae mbali na pumu.

11. Mbegu za Shamari ( kiungo jamii ya karoti)
Dawa mbadala zinazotibu pumuShamari

Tumia mbegu za shamari kila mara ili kujitibu na shambulio la asthma/pumu.

12. Maziwa ya moto
Ongeza kiasi sawa cha mafuta ya mzeituni na asali ndani ya kikombe cha maziwa ya moto. Kunywa mchanganyiko huu pamoja na punje mbili au tatu za kitunguu swaumu kabla ya chakula cha asubuhi kwa majuma kadhaa. Dawa hii ya asili inaponya pumu kwa haraka sana.

13. Majani ya Kotimiri
Dawa mbadala zinazotibu pumu
Kotimiri
Majani ya kotimiri (Parsley leaf) ni dawa mbadala nzuri sana kwa ajili ya kikohozi. Andaa chai ya majani haya na asali unywe kila siku. Itatibu kikohozi, itasafisha koo na kutibu pumu kadri siku zinavyosogea wakati ukiendelea kutumia chai hii kila siku
HITIMISHO .
kwa yeyote anaweza kutumia japo njia tatu hadi nne kwa mkupuo lakini changamoto ni namna ya kuchanganya hivyo ziko bidhaa ambazo tayari zimeandaliwa zenye mchanganyo wa vitu hivyo apo juu na zipo tayari kwa matumizi ukihitaji bidhaa hizo wasiliana na mwendesha blogg hii
                                                               Kwa mawasiliano piga

0756636990 au 0653148743


Dr Khalid Mzuka

Jumapili, 3 Aprili 2016

FAHAMU SABABU NA MATIBABU YA KUSAHAU SANA

                      Tokeo la picha la forgot


UTANGULIZI

      Kusahau sana ni hali inayoweza kumfanya mtu akajichukia sana, kukosa raha na kua na mawazo sana afanye nini kupambana na adha hiyo..

Hii ni hali ambayo inaathiri watu wengi sana yaani wakubwa na wadodo kulingana na chanzo lakini inakua mbaya zaidi mtu anavyozidi kuongezeka umri kwani seli za ubongo zinazidi kupungua zaidi.
Kuna hali kitaalamu inaitwa dementia ambayo hutokea mara nyingi katika umri mkubwa na huambatana na kusahau kuliko pitiliza yaani kupotea katika mazingira unayoyafahamu, kusahau majina ya kawaida kabisa kama embe, pazia, kiti na meza, kurudia kuuliza swali la aina moja kila siku, na kuchanganyikiwa lakini hali huu huletwa na magonjwa Fulani mfano Alzheimer's disease{hii hali ni hatari na hutibiwa kitaalamu}

Lakini watu wengi hawafiki huko, ila watu wengi sasa wanasahau vitu vya kawaida sana yaani unakuta mtu kaenda na baiskeli au gari sehemu afu karudi kwa mguu na kuvisahau huko, mtu anasoma sasa hivi afu akifunika kitabu amesahau, unaweka pochi sehemu unasahau uliweka wapi, unameza dawa afu baadae hukumbuki kama ulimeza au vipi, unasahau pesa mfukoni, unapewa kazi afu unasahau kuifanya na kadhalika..

BAADHI YA SABABU ZA KUSAHAU
Hali hizi sasa zinawatesa watu wengi na hawajui wafanye nini, lakini kuna tabia kadhaa ambazo zinaambatana na hali hizi kama ifuatavyo..

Kukosa usingizi:
 binadamu anatakiwa apumzike mpaka masaa nane kwa siku moja, lakini kutokana na ugumu wa maisha watu hujikuta wanalala mpaka masaa manne kwa siku. Hii huathiri uwezo wa kufikiri na kusahau kirahisi sana.

Madawa:
dawa zinazotibu magonjwa mbalimbali hua na madhara madogo madogo ambayo yanaleta kusahau.. mfano dawa za kutibu presha kama captopril, dawa za kutibu madonda ya tumbo mfano cimetidine na dawa za kutibu mgandamizo wa mawazo mfano amitriptyline.

Ulevi:
 unywaji wa pombe uliopitiliza huharibu uwezo wa kumbukumbu za mda mfupi yaani kusahau kitu umekifanya mda huo huo hivyo inashauriwa kunywa pombe kiafya. Yaani bia mbili kwa siku mwanaume na bia moja kwa siku mwanamke ambazo hazina alcohol zaidi ya asilimia tano zinatosha kiafya.

Mgandamizo wa mawazo:
 kitu chochote kinachokufanya ushindwe kutuliza akili, kitakufanya usahau sana na kushindwa kupata kumbukumbu ulizoziweka siku za nyuma.

Upigaji wa punyeto:
 tatizo hili la kusahau kwasababu ya punyeto ndio chanzo kikuuu kwa vijana wengi chini ya miaka 35 kwani tabia hii huambatana na maumivu ya kichwa, uchovu mwingi na kusahau kusiko kwa kawaida. 

Uvutaji wa sigara:
sigara ina kemikali iitwayo nikotini ambayo huenda kwenye ubongo na kuua seli za ubongo na kumfanya mtu asahau sana.

Kutokua makini
 tatizo la kufanya mambo haraka haraka huleta kusahau sana, kama wewe una mambo mengi amka mapema uyafanye ila ukianza kukimbia kimbia njiani ndio chanzo kikuu cha kusahau mambo mengine, pia tabia ya wanafunzi kusoma kwenye kelele sana au huku wanasikiliza mziki hujikuta hawaambulii kitu baada ya kufunika daftari.

Tokeo la picha la forgot


MATIBABU

Matibabu ya yasiyo ya dawa {non pharmacological treatment]
Kuacha tabia hizo juu ni njia bora zaidi ya kurudi katika hali yako ya kawaida japokua itakuchukua mda mrefu kidogo.lakini pia kuna njia za kufanya ili kuweza kukumbuka vitu baada ya kuacha tabia hizo hapo juu kama ifuatavyo.

Weka alarm; simu na saa nyingi zina alarm hivyo kama kuna kitu unataka kukifanya mda Fulani basi weka alamu ambayo ikiita tu utakumbuka sababu kwanini uliiweka.

Tumia kalenda: watu wengi tuna kalenda nyumbani lakini hatuzitumii. Kama una mpango wa kukutana na mtu Fulani siku mbele zijazo zungushia tarehe hiyo na kalamu itakusaidia kuona kila siku na kukumbuka.

Andika kwenye karatatasi; ukiamka asubuhi hebu andika mambo yote unayotegemea kuyafanya kwa siku nzima kisha weka mfukoni, hii itakusaidia kufanya vitu kwa mipango makini.

Fanya hicho kitu kitu sasa hivi: kama unataka kufanya kitu Fulani na hauna kazi nyingine kwa sasa basi kifanye sasa hivi ili usisahau tena baadae.

Tafuta mtu wa kukumbusha; anaweza kua mtu yeyote unayeishi nae, unaweza kumwambia mambo unayotaka kufanya ili awe anakukumbusha kila siku.

Usipokee kazi kama una kazi nyingi:mtu akikuomba msaidie kitu na unaona ratiba zako zimejaa kataa na umwambie ukweli kwani ukiikubali kazi hiyo utasahau..

Fanya mambo taratibu na umakini mkubwa: tabia ya kufanya vitu haraka haraka ndio hufanya mtu asahau sana, hebu kua makini na wakati mwingine jisemee moyoni. Mfano ukiweka simu kwenye droo sema moyoni ‘nimeweka simu kwenye droo’ itakusaidia kukumbuka.

tumia virutubisho:hivi ni virutubisho vinavyoongeza na kusaidia usambazaji wa damu kwenye ubongo wa binadamu, hutengenezwa na mimea asilia na havina kemikali kabisa.mfano ginkgo plus amabao ni mmea ambao hupatikana nchi za ulaya..mmea huu pamoja na kuongeza kumbukumbu hutumika kama ant aging huku nchi za uchinna yaani huchelewesha mtu kuonekana mzee. dose ya virutubisho hivi ni kimoja kwa mwezi.

kwamaelezo zaidi mtafute muongoza blogu kwa mawasiliano yake



Kwa mawasiliano piga

0756636990 au 0653148743


Dr Khalid Mzuka

Jumamosi, 26 Machi 2016

ELEWA LEO KUHUSU YELLOW FEVER/HEPATITIS B (HOMA YA MANJANO)




UTANGULIZI.
Ugonjwa    wa Manjano    ambao hufahamika kitaalamu  kama HEPATITIS  B  ni hatari  sana  na umesababisha vifo  vya  mamilioni  ya  watu  duniani  kote.  Kwa  mujibu  wa ripoti  ya  Shirika  la  Afya  Duniani  (W.H.O)   kuna  zaidi ya watu Milioni  350  duniani  ambao  wameathiriwa  na  ugonjwa  huu hatari   kabisa  na  zaidi  ya  watu  620,000  hufa  kila  mwaka  kwa ugonjwa  wa Manjano.
CHANZO   CHA  UGONJWA  WA  MANJANO
Ugonjwa  wa  Manjano  husababishwa  na  virusi  viitwavyo  “ Hepatitis  B “ (HBV)  ambavyo  hushambulia zaidi ini  la mwanadamu. Virusi  hivi  visipo  tibiwa  mapema  hutengeneza uvimbe  katika  ini  na  kusababisha  saratani ya ini (livercancer) ambayo hupelekea  kifo.
 
MAAMBUKIZI  YA  UGONJWA WA  MANJANO.
Ugonjwa    wa  Manjano  huambukizwa  kwa  njia  zifuatazo  :
i.                   Kujamiiana  bila  kutumia  kinga.
ii.                Kunyonyana  ndimi
iii.             Kuchangia  damu  isiyo  salama
iv.             Mama  mjamzito mwenye  ugonjwa  huu  anaweza kumuambukiza  mtoto  wake  wakati  wa  kujifungua.
v.                Kuchangia  vitu  vyenye  ncha  kali  kama  vile  wembe  na sindano.

                        DALILI  ZA  UGONJWA  WA  MANJANO
Dalili  za  ugonjwa wa  manjano  huchukua  muda  mrefu kuonekana  tangu  maambukizi  yatokee, na  zinapo  anza kuonekana  wazi  wazi, mgonjwa  anakuwa  amesha  athirika  kwa kiwango  kikubwa  sana.  Dalili  za  ugonjwa   huu  ni  kama ifuatavyo :
i.                     Uchovu  wa  mwili
ii.                Kichefuchefu
iii.             Mwili  kuwa  dhaifu
iv.             Homa  kali
v.                 Kupoteza  hamu  ya  kula
vi.             Kupungua  uzito
vii.          Kupatwa  na  maumivu  makali  ya  tumbo upande  wa  ini.
viii.       Kukojoa  mkojo  wa  rangi  nyeusi
ix.              Macho  na  ngozi  kuwa  vya  njano.

KINGA   YA  UGONJWA  WA  MANJANO
i.                    Kupatiwa  chanjo  ya  kujikinga  na  maambukizi  ya ugonjwa  huu.
ii.                Kutumia  kinga  wakati  wa  kujamiiana
iii.             Kuacha   kuchangia  vitu  vyenye  ncha  kali  kama  sindano, wembe  n.k
iv.             Kutochangia  mswaki
v.                Kuwa  na  mpenzi  mmoja  mwaminifu
vi.             damu  ambayo  haijapimwa  na  kuthibitika kuwa  salama isiongezwe kwako (transfussion)

                     TIBA   YAKE MAHOSPITALINI  
Ugonjwa  wa  manjano  hauna  tiba  isipokuwa  mgonjwa   akiwahi hospitali  atapatiwa  dawa za  kupambana  na  virusi  kuvipunguza nguvu  za  kupambana  na  ini., kupandikizwa  ini  ambapo ini lililoathirika  huondolewa  na  kuwekwa  jingine  japo  ni  vigumu kupata  ni  salama.
Ukisha  gundua  kuwa  umeambukizwa  ugonjwa  huu unashauriwa   kuacha  kutumia  pombe, dawa  za  kulevya  na  vitu vingine  vinavyo  athiri  utendaji  kazi  wa  ini.

TIBA YA ASILI KWA MIMEA
kuna baadhi ya mimea imekua ikisaidia sana mwanzo kwa kupunguza kasi na kuugulia dalili zoote na baadae kuumaliza kabisa ugonjwa huu lakini ufafanuzi wa mimea hii na namna ya kuichanganya wasiliana na muendesha blogu hii kwa simu ya kawaida (kupiga)

piga simu namba

0756636990 au 0653148743

Dr Khalid Mzuka