Alhamisi, 25 Februari 2016

HIZI NDIO NJIA SABA ZA KUACHA PUNYETO KABISA...

Karibuni tena wapendwa wasomaji wa blog hii ya afya na maisha bora na kama kawaida leo tena unapata shule nyingine ambayo namatumaini inaendelea kukujenga kiakili na kiafya..
Makala iliyopita niliongelea madhara yanayosababishwa na kupiga punyeto kama hukusoma hii hapa .HAYA NDIO MADHARA KUMI YA KUPIGA PUNYETO…..{ MASTURBATION}lakini nilipokea simu nyingi ambazo zilitaka pia niongelee suluhisho au jinsi gani mtu anaweza kuacha punyeto kabisa
Punyeto kama tulivyoongea ni tatizo la tabia na linaweza kudhibitika kabisa kama matatizo mengine yeyote. FANYA YAFUATAYO....                                                   
  •  Acha kuangalia video za ponograph: video hizi ndio chanzo  kikuu cha punyeto kwa watu wengi hua zinajenga picha nyingi kwenye ubongo  na kila picha unayoiona utataka ukaipigie punyeto hivyo  kuacha kuziangalia tu ndio nafuu yako..                                                                                                                                                                            Weka mipango ya kuzuia kupiga punyeto wakati wa kuoga:bafuni ndio sehemu ambayo inatumika sana na watu wengi kupiga punyeto hivyo ni vizuri kua na mikakati ya kujizuia ukiwa huko kwa kuoga haraka na kuondoka, kuoga maji ya baridi ambayo mara nyingi hayatoi muhemko wa kupiga punyeto.
  •  Epuka kukaa nyumbani peke yako; mara nyingi kukaa peke yako kunakufanya ushawishike kufanya tendo hilo, hebu ondoka na ujichanganye na watu wengine au tafuta majirani wa kukaa na kuongelea mambo mengine.
  • Fikiria kuhusu madhara yake: kila aliyewahi kupiga punyeto kuna madhara mabayo ameshayapata hasa madogo madogo kama uchovu mkubwa, kuumwa kichwa na kusahau sana hii itakupa moyo wa kuendelea kutopiga punyeto.
  • acha kusema eti hii punyeto ni ya mwisho: siku zote wapiga punyeto wana akili moja ya kufikiria eti sasa leo napiga afu sirudii tena. Hicho kitu hakipo, kwani kesho yake utasema ivoivo, kama unaacha acha mara moja.
  • Tafuta mpenzi kama huna kabisa: ukiwa na mpenzi madhara ya punyeto kama kupungukiwa nguvu za kiume yatakufanya uache kabisa kwani ukiendelea utaaibika siku moja pale uume utakaposhindwa kusimama kabisa mkiwa faragha chumbani na pia utapata nafasi ya kushiriki tendo la ndoa hivyo kuacha kabisa punyeto. pia unaweza kumshirkisha mwenzi wako tatizo lako ili akusaidie kuacha.
  • anza mazoezi na jishughulishe na mambo mengine:hii itakufanya ue bize na mambo mengine na utumie mda wako mwingi huko,  pia mazoezi ya jioni yatakufanya uchoke na kushindwa kufikiria kupiga punyeto wakati wa kwenda kulala.
  • hapo ndio mwisho labda tu baada ya siku mbili ntatoa maelezo kuhusu namna ya kuongeza nguvu za kiume kwa waliothiriwa na punyeto au walioathiriwa na vitu vingine vingi.
kwa mawasiliano piga simu namba
0756636990 au 0653148743

khalid J Mzuka

Jumanne, 23 Februari 2016

HAYA NDIO MADHARA KUMI YA KUPIGA PUNYETO…..{ MASTURBATION}

Punyeto ni nini?
Hii ni tabia ambayo mwanamke au mwanaume anajichua sehemu za siri ili kufika kileleni, mara nyingi kitendo hiki hufanyika na muhusika akiwa peke yake chumbani au bafuni.
Wahanga wengi wa tabia hii ni wanaume kwani huanza katika umri mdogo sana kwasababu ya uoga wa kufuata wasichana na kuangalia video za ngono ambazo huwasukuma kufanya vitendo hivi..
Lakini punyeto huambatana na madhara makubwa ya kijamii na kiafya na leo tutaangalia madhara hayo kumi ya punyeto..


  1. 1.       Punyeto humfanya mtu awe mlegevu bila kua na nguvu kabisa mda wote kwani nguvu nyingi sana hutumika kwenye tendo hili.
  1. 2.       Ni moja ya chanzo kikuu cha kupoteza nguvu za kiume kwasababu ya kuharibu mishipa ya fahamu wakati mtu akijisugua.
  1. 3.       Punyeto hupunguza idadi ya mbegu za kiume{low sperm count} hivyo ni mbaya sana kwa wapenzi wanaotafuta mototo.
  1. 4.       Husababisha mtu kusahau sana na kushindwa kufanya vitu kwa makini zaidi.
  1. 5.       Humfanya mtu awe mchovu mda wote na kusinzia ovyo kila anapomaliza kupiga punyeto.
  1. 6.       Husababisha mwanaume kutoa mbegu haraka kipindi cha tendo la ndo na kushindwa kumfikisha mwanamke kileleni..{pre mature ejaculation}
  1. 7.       Husababisha msongo mkubwa wa mawazo kwani kila ukimaliza tendo hilo unajuta sana na kuapa kwamba hutarudia tena.
  1. 8.       Huleta utumwa wa kifikra kwani ukishaanza huwezi kuacha kirahisi{ addiction}
  1. 9.       Punyeto husababisha mwanaume au mwanamke kukosa hamu kabisa na mwenza wake hivyo kuleta usumbufu kwenye mahusiano.
  1. 0.   Punyeto ni chanzo kikuu cha ngono za jinsia moja shuleni na vyuoni ambazo huambukiza magonjwa ya zinaa kama kaswende, gono na ukimwi kirahisi sana.

kama umeshindwa kabisa kuacha nitafute kwa simu au fatilia makala ijayo baada ya siku mbili mbele

                              piga simu 0756636990/0653148743
                                khalid Mzuka

Jumapili, 21 Februari 2016

KAMA WEWE NI MMOJA YA BAADHI YA WANAUME WANAOTAFUTA DAWA YA KUONGEZA MAUMBILE YAO YA KIUME SOMA HAPA ..

utangulizi
Kwa miaka mingi wanaume wengi wamekua wakijihisi wana nyeti ndogo kulingana  hadithi wanazosikia mtaani kuhusu wanaume wengine wenye maumbile makubwa, video za phonograph,na tabia za kuoga pamoja hasa shule za bweni kipindi cha masomo ya sekondari.
Kampuni zizodai zinaweza kuongeza maumbile ya kiume zimetengeneza pesa nyingi sana kwa kudai zina vidonge, sindano, na  dawa za asili kwa ajili ya kazi hii.
Uchunguzi wa kisayansi uliofanyika india umegundua zaidi ya 60% ya wanaume wana wasiwasi na maumbile ya nyeti zao.
Leo naomba nikutoe dukuduku la  mawazo yako wewe msomaji wa kiume ambaye na wewe unadhani una maumbile madogo na unatafuta suluhisho.
  
Je ni kweli una maumbile madogo?
Jibu ni hapana, kwani ukijiangalia mwenyewe  angle unayotumia kujiangalia inakufanya ujihisi una maumbile madogo, lakini mwanaume unayelingana nae maumbile akisimama mbele yako utaona anakuzidi mbali sana kulingana angle uliyosimama kumuangalia yeye.

Je maumbile ya kawaida yanalinganaje?
Kosa kubwa linalofanywa na wanaume ni kujipima urefu wa maumbile yao wakati yakiwa yamesinyaa.
 lakini naomba nikwambie kipimo halali cha uume ni pale uume unapokua umesimama tu.
Nyeti mbili zilizosinyaa zinaweza kuonekana zinatofautiana urefu, mfano moja ikawa na sentimita sita na nyingine tisa lakini zikisimama zote zikafika sentimita 15.
Utafiti umeonyesha mwanaume wa kawaida ana  uume wenye urefu  sentimita 12 mpaka 15 na unene{circumference} wa sentimita 12  akiwa amesimamisha.
 zaidi ya asilimia 95% ya wanaume wamo kwenye hicho kiwango hicho.
 Japokua kuna wanaume wanakua na uume mkubwa kidogo kuliko vipimo nilivotaja hapo juu lakini uume ni sawa na viungo vingine vya binadamu kama mguu na mikono  na haviwezi kua sawa kabisa.
Lazima kuna watu wana miguu au viganja vya mikono  vikubwa kidogo kuliko wengine.
 Ni 0.6% ya wanaume wanaoupatwa na hali inayoitwa kitaalamu kama micro penis ambayo uume husimama kwa sentimita saba tu.
Hali hii husababishwa mara nyingi na kuepo kwa kiwango kidogo sana cha hormone inayoitwa  growth hormone kipindi cha ukuaji.
Hali huweza kutibiwa na wataalamu wa nyeti{urologist}  bila madhara yeyote.


Mahusiano kati ya tendo la ndoa na ukubwa wa maumbile ya kiume.
Utafiti uliofanyika na mtafiti wa kimarekani kwa jina la jonson uligundua wanawake wengi hua swala la ukubwa au udogo wa maumbile halipo vichwani mwao na sio kesi kubwa kama wanaume wengi wanavyolichukulia.
Swala la kumridhisha mwanamke halina mahusiano na urefu wa uume japokua baadhi ya wanawake walikiri kuridhishwa kirahisi na wanaume wenye uume mnene na sio mrefu kama watu wengi wanavyofikiria.
Lakini point yangu hapo juu haimaanishi wanaume wenye uume mwembamba hawawezi kuwaridhisha wanawake. La hasha.
Lakini pia naomba nikuonye wewe mwanamke unayesoma hapa usije ukamwambia mpenzi wako ana maumbile madogo ata kama unatania.
Kauli hyo ataichukulia uzito mkubwa na itamuumiza sana kichwa kuliko unavyofikiria.
     
Je kuna dawa ya kuongeza nyeti za kiume?
 Mpaka sasa hivi, Hakuna dawa yeyote ambayo imethibitishwa kuongeza nyeti za kiume kama makampuni mengi yanavyodai.
Ni operation  na mazoezi tu ndio yamefanikiwa kuongeza maumbile kwa sentimita tatu mpaka tano na zimekua zikiambatana na madhara makubwa kama kubadilika kwa shape za nyeti, kupungukiwa nguvu za kiume, kuchelewa kupona na maumivu ya mda mrefu hasa kawa oparesheni.{chronic pain}
hata hivyo mazoezi ya kuongeza uume yameonekana hayana madhara kabisa.
Zaidi ya 75% ya wanaume waliofanyiwa operation hzo hawakuridhika na matokeo yake hivyo sikushauri na wewe uingie huko labda kama una ugonjwa wa micropenis nilioutaja hapo juu.
Mwisho nakuomba wewe mwanaume ufahamu kwanzia leo kwamba hayo maumbile yako hayana matatizo yeyote na wewe ni dume la mbegu.
                           

                                 kwa mawasiliano piga simu  0756636990 au 0653148743