Jumamosi, 26 Machi 2016

ELEWA LEO KUHUSU YELLOW FEVER/HEPATITIS B (HOMA YA MANJANO)




UTANGULIZI.
Ugonjwa    wa Manjano    ambao hufahamika kitaalamu  kama HEPATITIS  B  ni hatari  sana  na umesababisha vifo  vya  mamilioni  ya  watu  duniani  kote.  Kwa  mujibu  wa ripoti  ya  Shirika  la  Afya  Duniani  (W.H.O)   kuna  zaidi ya watu Milioni  350  duniani  ambao  wameathiriwa  na  ugonjwa  huu hatari   kabisa  na  zaidi  ya  watu  620,000  hufa  kila  mwaka  kwa ugonjwa  wa Manjano.
CHANZO   CHA  UGONJWA  WA  MANJANO
Ugonjwa  wa  Manjano  husababishwa  na  virusi  viitwavyo  “ Hepatitis  B “ (HBV)  ambavyo  hushambulia zaidi ini  la mwanadamu. Virusi  hivi  visipo  tibiwa  mapema  hutengeneza uvimbe  katika  ini  na  kusababisha  saratani ya ini (livercancer) ambayo hupelekea  kifo.
 
MAAMBUKIZI  YA  UGONJWA WA  MANJANO.
Ugonjwa    wa  Manjano  huambukizwa  kwa  njia  zifuatazo  :
i.                   Kujamiiana  bila  kutumia  kinga.
ii.                Kunyonyana  ndimi
iii.             Kuchangia  damu  isiyo  salama
iv.             Mama  mjamzito mwenye  ugonjwa  huu  anaweza kumuambukiza  mtoto  wake  wakati  wa  kujifungua.
v.                Kuchangia  vitu  vyenye  ncha  kali  kama  vile  wembe  na sindano.

                        DALILI  ZA  UGONJWA  WA  MANJANO
Dalili  za  ugonjwa wa  manjano  huchukua  muda  mrefu kuonekana  tangu  maambukizi  yatokee, na  zinapo  anza kuonekana  wazi  wazi, mgonjwa  anakuwa  amesha  athirika  kwa kiwango  kikubwa  sana.  Dalili  za  ugonjwa   huu  ni  kama ifuatavyo :
i.                     Uchovu  wa  mwili
ii.                Kichefuchefu
iii.             Mwili  kuwa  dhaifu
iv.             Homa  kali
v.                 Kupoteza  hamu  ya  kula
vi.             Kupungua  uzito
vii.          Kupatwa  na  maumivu  makali  ya  tumbo upande  wa  ini.
viii.       Kukojoa  mkojo  wa  rangi  nyeusi
ix.              Macho  na  ngozi  kuwa  vya  njano.

KINGA   YA  UGONJWA  WA  MANJANO
i.                    Kupatiwa  chanjo  ya  kujikinga  na  maambukizi  ya ugonjwa  huu.
ii.                Kutumia  kinga  wakati  wa  kujamiiana
iii.             Kuacha   kuchangia  vitu  vyenye  ncha  kali  kama  sindano, wembe  n.k
iv.             Kutochangia  mswaki
v.                Kuwa  na  mpenzi  mmoja  mwaminifu
vi.             damu  ambayo  haijapimwa  na  kuthibitika kuwa  salama isiongezwe kwako (transfussion)

                     TIBA   YAKE MAHOSPITALINI  
Ugonjwa  wa  manjano  hauna  tiba  isipokuwa  mgonjwa   akiwahi hospitali  atapatiwa  dawa za  kupambana  na  virusi  kuvipunguza nguvu  za  kupambana  na  ini., kupandikizwa  ini  ambapo ini lililoathirika  huondolewa  na  kuwekwa  jingine  japo  ni  vigumu kupata  ni  salama.
Ukisha  gundua  kuwa  umeambukizwa  ugonjwa  huu unashauriwa   kuacha  kutumia  pombe, dawa  za  kulevya  na  vitu vingine  vinavyo  athiri  utendaji  kazi  wa  ini.

TIBA YA ASILI KWA MIMEA
kuna baadhi ya mimea imekua ikisaidia sana mwanzo kwa kupunguza kasi na kuugulia dalili zoote na baadae kuumaliza kabisa ugonjwa huu lakini ufafanuzi wa mimea hii na namna ya kuichanganya wasiliana na muendesha blogu hii kwa simu ya kawaida (kupiga)

piga simu namba

0756636990 au 0653148743

Dr Khalid Mzuka

Ijumaa, 18 Machi 2016

ONGEZA MAKALIO KWA LISHE NA MAZOEZI NA SIO KICHINA

miaka ya hivi karibuni kua na makalio makubwa imekua ni fasheni muhimu sana kiasi kwamba wanawake wasio na makalio makubwa wamejikuta wakipata tabu na hata kufanya upasuaji hatari ili kuongeza makalio na wengi wameharibika kabisa au kupoteza maisha kwenye oparesheni hizo hatari. lakini kama jinsi wanaume wanavyobeba vyuma na kuongeza vifua na mikono hivyohivyo wanawake wanaweza kuongeza misuli hiyo muhimu ya makalio ambayo kitaalamu inaitwa gluteal maximus    ,gluteal minimus na gluteal medias.

 hiyo ndio misuli mikuu mitatu ambayo kwa pamoja inaitwa makalio na ikifanyiwa mazoezi vizuri huongezeka na kua mikubwa. ni kweli ukubwa wa makalio na kiungo chochote cha mwili hufuata ukoo lakini pia mazoezi husaidia sana kukuza makalio au kiungo chochote cha mwili chenye misuli lakini sio kua makubwa tu lakini hata kuyafanya kua na shepu nzuri na kuvutia.. unaweza kua hujaamini bado lakini kwa kukuthibitishia habari hizi ni kwamba jeniffer lopez mwanamuziki na muigizaji wa filamu nchini marekani ambaye anaongoza kwa kua na makalio makubwa zaidi kuliko wasanii wote mpaka akayakatia bima yaani insurance anafanya mazoezi haya kama ifuatavyo..


mazoezi ya squat;
mazoezi haya huanzwa kwa kusimama na miguu yote miwili kisha kuanza kama unakaa hewani halafu unainuka, mazoezi haya huvuta misuli ya makalio na kuibana kisha kuongeza upana na siku za kwanza za mazoezi haya mtu hujisikia maumivu na kuanza kuhisi nguo zimeanza kubana mpaka mapajani. ni zoezi kuu na muhimu katika kukuza makalio.fanya zoezi hili kwa raundi tatu kila raundi fanya mara kumi na tano au unaweza ukaanza kama picha inavyoonyesha hapo kwa mwezi mmoja kisha ukaendelea na mazoezi ya kawaida kama nilivyoelekeza.


 zoezi la bridge;
watu wengi wanashinda wamekaa kwenye viti  mashuleni au maofisini muda mwingi na hali hii hufanya hata mtu mwenye makalio makubwa ya kuzaliwa nayo kuanza kupoteza shepu yake nzuri ya mwanzoni. zoezi hili huanza kwa kulala chini kwa mgongo kisha inua kiuno kwa juu, sasa bakia kwa hali hii kwa muda kisha nyoosha mguu mmoja kwa mbele kwa sekunde kadhaa afu rudisha chini halafu badilisha mguu.fanya hivi kwa kila mguu mara kumi kwa raundi tatu huku ukipumzika dakika mbili kila baada ya raundi.

 donkey kick;
piga magoti kisha weka mikono chini kama mbuzi anavyosimama kisha inua mguu mmoja wa nyuma mpaka uangalie juu kisha rudisha chini taratibu.fanya hivi raundi tatu huku kila mguu ukiinua na kuurudisha mara 20.


kula protini nyingi:
vyakula vya protini ni muhimu kujenga misuli na mifupa hivo kula sana maharage, nyama, samaki,maziwa, karanga, korosho na kadhalika. hii itakujenga haraka sana na kukupa matokeo mazuri kwani mwili unajengwa na chakula.




 chagua aina nzuri ya wanga;
 ulaji wa mikaango kama chips, chapati, maandazi na kadhalika sio wanga nzuri kwani huleta vitambi na kukufanya ue na shepu mbaya ni vizuri kula wanga asili kama ugali,viazi,mihogo,wali na kadhalika.






tumia mboga za majani; mboga za majani ni muhimu sana kwani husaidia chakula ulichokula kiweze kunyonywa na mwili kirahisi na kupunguza uwezekanao wa kupata kitambi.





tumia virutubisho vya kutosha;

virutubisho vyenye madini mbalimbali na protini ni muhimu sana kwani vyenyewe vinaenda moja kwa moja kufanya kazi kwenye mwili na kuanza kujenga misuli hii bila kuanza kufyonzwa taratibu tumboni kama vyakula vingine. utafiti unaonyesha wanaotumia virutubsho hivi hufanikiwa sana kuliko wasiotumia kabisa.jinsi ya kutumia; chota kijiko kimoja kilichowekwa kwenye virutubisho vyako kisha changanya na maziwa kwa upande wa protein shake na kwa upande wa argi changanya kijiko kimoja cha unga na maziwa ya mgando au juice.kunywa mara moja au mbili kwa siku huku ukiendelea na mazoezi.


 


mwisho: kama ilivyokua kwa mazoezi mengine yeyote itakuchukua muda angalau wiki mbili au mwezi mmoja kuanza kuona matokeo na haimaanishi kwamba ndio matokeo mazuri yakipatikana ndio unaacha hapana, mazoezi ni muhimu kwa mwili wa binadamu, unaweza ukaanza na zoezi la mwezi yaani mara moja kwa siku kisha endelea na zoezi hili mara tano kwa wiki baada ya mwezi wa kwanza. kumbuka kama ilivyo kwa mazoezi mengine ya mwili, unahitaji moyo wa mazoezi kufanikiwa, usije ukafanya zoezi siku mbili ukaacha afu ukategemea mabadiliko..unaweza ukatutafuta kupata virutubisho hivyo, kupata video za mazoezi na kwa msaada wa kitaalamu zaidi.


piga simu namba

0756636990 au 0653148743

Dr Khalid Mzuka

Jumanne, 15 Machi 2016

ELEWA VIZURI OVARIAN CYST (UVIMBE KATIKA MAYAI YA MWANAMKE)

OVARIAN CYST NI NINI?? 
           Ni uvimbe unaotokea katika mayai ya mwanamke (ovarian). uvimbe huo hutokana na mkusanyiko wa maji maji yanayozungukwa na kutu nyembamba ndani ya mayai ya mwanamke, uvimbe huu hutokea kwa wanawake wa rika tofauti na mara nyingi huonekana kwa wanawake waliofika umri wa kushika ujauzito, uvimbe huu huweza kuwa na ukubwa wa cm3_cm30 na unaweza kujaza tumbo lote 

AINA ZA UVIMBE KATIKA MAYAI YA MWANAMKE 


  • HEMORRHAGIC CYST

hii ni Aina ya uvimbe ambayo hutokea wakati kukiwa na uvujaji wa damu ndani ya uvimbe wa Aina yoyote ule ambao umeshajitengeza tayari,pia uvimbe huu huambatana na maumivu makali kwenye upande mmoja wa ubavu (kushoto /kulia) 

  • FOLLICULAR CYST

hii ni Aina ya uvimbe unaotokea wakati ovulation isipotokea au baada ya corpus luteum kuanza kusinyaa na kupotea yenyewe baada ya kutopachikwa kwa yai kwenye kuta za mfuko wa kizazi, pia uvimbe huu una ukubwa wa wastani 2:3 kwa upana, uvimbe huu hauna dalili yoyote na hupotea yenyewe baada ya Muda 
  • CORPUS LUTEUM 
hii ni Aina ya uvimbe ambazo unatokana na kutopachikwa kwa yai la uzazi lililorutubishwa na mbegu ya kiume kwenye mfuko wa kizazi, pia uvimbe huu husinyaa na kupotea wenyewe ingawa wakati mwingine huweza kujaa maji na kusababisha tumbo kuvimba upande mmoja 
  • DERMOID CYST 
uvimbe huu hujulikana kama MATURE CYST TERATOMA, huathiri wanawake wadogo walio katika umri wa kushika ujauzito na uvimbe huu huweza kukua nchi 6 kwa upana na ndani Yake huweza kuwa na mchanganyiko wa nywele, mifupa, mafuta na cartilage, pia uvimbe huu huweza kuwa mkubwa zaidi na kujizungusha hivyo huathiri mzunguko wa damu na hivyo kusababisha maumivu makali ya nyonga na tumbo. 
  • POLYCYSITIC APPEARING CYST
huu ni uvimbe mkubwa sana na huwa umezungukwa na vijiuvimbe vidogo vidogo na huonekana hata kwa wanawake wenye Afya njema na wale wenye tatizo la homorne
  • CYSTEDENOMA 
hii ni Aina ya uvimbe ambayo hutokea kwenye tissue za ovary na hujazwa na maji maji Aina ya kamasi pia uvimbe huu una ukubwa wa nch, 12 au zaidi kwa upana 
  • ENDOMETRIOSIS 
huu ni uvimbe unaosababishwa na uwepo wa Aina mojawapo ya kuta za mfuko wa kizazi unaojulikana kama ENDOMETRIUM kwenye mayai ya mwanamke, uvimbe huu huathiri wanawake walio katika umri wa kushika ujauzito na huambatana na maumivu makali (sugu) ya nyonga (CHRONIC PELVIC PAIN) wakati wa hedhi, pia uvimbe huu una rangi nyekundu ya kahawia (reddish brown) na una ukubwa wa 0.75_8 inches

VIHATARISHI VYA TATIZO HILI 
👉1. kuwa na mzunguko wa hedhi usioeleweka (IRREGULAR MENSTRUATION CYCLE) 
👉2. kuwa na mafuta mengi tumboni
👉3. kukosekana kwa uwiano wa vichocheo mwilini (hormone imbalance) 
👉4. kuvunja ungo mapema yani kuanzia miaka 11kushuka chini 
👉5. kutumia dawa za kemikali maana zina side effects
 
DALILI NA VIASHIRIA VYA TATIZO HILI 

   
A. mwanamke kupata maumivu /kichomi ambayo huwa hayana Muda maalumu huchoma ukeni,                kiunoni, mgongoni, mapaja, NK
 
👉B. kuhisi tumbo kuwa zito limejaa au kuvimba 
👉C. kupata maumivu makali katika matiti 
👉D. kutopata hedhi katika mpangilio 
👉E.  kuongezeka uzito mara kwa mara 
👉F.  kupata maumivu katika mbavu 
👉G. kuumwa kichwa mara kwa mara 
👉H. nywele kukua haraka kila wakati 
👉I.  kupata maumivu makali wakati wa hedhi 
👉J. kuhisi kichefchef (kutapika) 
👉K. kupata maumivu makali ya nyonga 
👉L. kuhisi uchovu kila wakati 
👉M. kutokwa na matone ya damu 
👉N. kutoshika mimba 
👉O. mabadiliko katika upatikanaji wa haja 
               a. haja ndogo kutoka Bila kujielewa 
               b haja kubwa kuwa ngumu 

VIPIMO NA MATIBABU 

Matibabu hufanyika kwa kuangalia Majibu yaliyopatikana katika vipimo, Kuna vipimo vingi vya kuona tatizo hili kama vile ENDOVAGINAL ULTRA SOUND, COMPLETE BLOOD COULD, SERUM CA 125 ASSAY, URINE FOR PREGNANCY, baada ya daktar kupata Majibu ndio huangalia tiba inayoendana na Majibu yaliyopatikana katika vipimo mbalimbali, matibabu hayo huweza kuwa ya Aina mbili 
(@)MATIBABU YA DAWA 
~tiba hii huhusisha matumizi ya dawa za upangaji uzazi kwa Muda wa wiki 4_6, matumizi ya dawa Hizi kwa Muda mrefu huzuia kutokea tena uvimbe katika kizazi kwasababu dawa Hizi hufanya Kazi ya kuzuia mayai kutotoa mayai ya uzazi (ovums) pia dawa Hizi hazipunguzi uvimbe uvimbe kwasababu uvimbe utapotea wenyewe baada ya Muda 
(B) TIBA YA UPASUAJI
katika tiba hii ya upasuaji Kuna Aina mbili 
                    (1)EXPLORATORY LAPARATOMY 

~katika tiba hii mgonjwa hupasuliwa tumboni na daktar huweza kuondoa uvimbe, upasuaji huu hufanyika kwa mwanamke mwenye uvimbe ambao hauwezi kupotea na mkubwa kuanzia 5cm_10cm
                     (2)LAPARASCOPIC SURGERY

~huu ni upasuaji ambao daktari hupasua sehem ndogo na kutumbukiza mpira maalumu ambao una kamera kwa mbele na huondoa uvimbe katika mayai, upasuaji huu hupendwa na wanawake wengi kwasababu hauachi kovu lolote na mara nyingi hufanyika kwa uvimbe mmoja 

ZINGATIA hakikisha unaenda kupima Afya yako mara nyingi kwani Kuna watu wapo na tatizo hili ila wanashindwa kuelewa au hawajitambui hivyo ni bora ukaepuka ugonjwa huu kwani madhara Yake ni kusababisha UGUMBA 
zimeonekana bidhaa zetu za asili kusaidia sana tangu miaka ya 1996 kwa waliofanyiwa upasuaji wa namna zote na zinasaidia pia kurutubisha mayai kwa usalama na zinafaa pia kutumiwa na mtu asiye na tatizo kwani sio dawa za matibabu ila ni virutubisho muhimu kwa tatizo hilo wasiliana nasi kuzipata bidhaa zetu 
 
piga simu namba

0756636990 au 0653148743

Dr Khalid Mzuka